Psalms 74:3-10

3 aGeuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,
uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.

4 bAdui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.
5 cWalifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.
6 dWalivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.
7 eWaliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.
8 fWalisema mioyoni mwao,
“Tutawaponda kabisa!”
Walichoma kila mahali ambapo Mungu
aliabudiwa katika nchi.
9 gHatukupewa ishara za miujiza;
hakuna manabii waliobaki,
hakuna yeyote kati yetu ajuaye
hali hii itachukua muda gani.

10 hEe Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?
Je, adui watalitukana jina lako milele?
Copyright information for SwhNEN